Hatua za awali za ukarabati kuelekea uwekaji wa nyasi bandia kwenye uwanja mkongwe wa Nyamagana Jijini Mwanza unaendelea vizuri ambapo leo ni siku ya pili tokea zoezi hilo lianze.
![]() |
| Uwanjwa wa Nyamagana katika ukarabati |
Wakuganda in sports imeshuhudia hii leo asubuhi jinsi Jassie and Company Limited ( JASCO) ambayo
imepewa kazi hii ya ukarabati wa uwanja huo, ikiendelea vema ikiwa ni pamoja na kazi ya kuchimba
udongo sehemu ya kuchezea (Pitch)
Kwa mujibu wa kampuni ya ushauri wa kitaalamu (ACT Global
Consultancy) ya nchini Marekaniambayo inasimamia zoezi hilo kwa niaba ya
shirikisho la soka ulimwenguni – FIFA, zoezi linakwenda vizuri na wananchi wa
Mwanza na Tanzania kwa ujumla wasubirie kuona uwanja wa Nyamagana ukiwa kwenye
hadhi ya kipekee.
“Sisi tuko makini na hatuna mchezo kwenye kazi. Tunasimamia
ujenzi huu na kupeleka taarifa FIFA. Tutahakikisha tunafanya kazi hii vizuri
ili kujijengea kupata kazi zingine FIFA” amesema mmoja wa wahandisi wa kampuni
ya ACT Global Bibonimana Dieudonne.
Aliongezea kuwa
katika hatua za awali miongoni mwa kazi zitakazotekelezwa ni kuchimba
udongo, kuweka changarawe, kuweka kokoto, kushindilia udongo,kuweka mabomba kwa
ajili ya kupitisha maji.
Hii sio mara ya kwanza kwa kampuni hiyo chini ya mpango wa
FIFA Goal Project kufanya kazi ya ushauri wa kitaalam kwani tayari kwani tayari
imesimamia ujenzi wa viwanja chi za Chad, Misri, Malawi, Burundi,Jamhuri ya
kidemocrasia ya Kongo.
Bibomana ameahidi kuwa ndani ya miezi miwili kazi ya uwekaji
wa nyasi bandia itakuwa imekamilika endapo tu kama FIFA itatumia wajibu wake
kwa kutuma pesa kwa wakati sambamba na vifaa.
![]() |
| Isaacki wakuganda-wakuganda in sports (kushoto) akihojiana na Bibonimana Dieudonne (mhandisi kutoka kampuni ya ACT Global Consultancy) |
Siku za hivi karibuni yalibuka maswari mengi kuhusu uwekaji
wa nyasi bandia kwenye uwanja wa huo kutokana na zoezi hilo kuchukua muda mrefu
bila mchakato wake kuanza. Lakini sasa kila kitu kiko wazi.
![]() |
| Uchimbaji udongo katika uwanja wa Nyamagana |
Ili kufanikisha zoezi hilo la Uwekaji wa nyasi bandia katika Uwanja huo wa Nyamagana, FIFA ilitoa kiasi cha dola za Marekani 500,000 ambapo Halmashauri ya Jiji la Mwanza ambao ndiyo wamiliki wa uwanja huo, imechangia kiasi cha dola 118,000 (Sh milioni 295) kama mchango wake kwa ajili ya zoezi hilo ambalo linatarajiwa kugharimu dola 618,000 (Sh milioni 988).
![]() |
| Zoezi la uchimbaji udongo - uwanja wa Nyamagana |
Uwanja wa Nyamagana utakuwa ni uwanja wa nne kuwekewa nyasi hizo za bandia hapa nchini ambapo tayari viwanja vya Uhuru na Karume vya jijini Dar es Salaam na Migombani cha Zanzibar vimewekewa nyasi hizo huku Uwanja wa Kaitaba Mkoani Kagera nao ukiwa ni Miongoni mwa Uwanja ulio katika orodha ya kuwekewa nyasi bandia na hivyo kuongeza idadi ya viwanja vyenye nyasi bandia hapa nchini.
![]() |
| Ofisi ya chama cha mpira wa miguu Wilaya ya Nyamagana |






0 comments:
Post a Comment