Mchezo wa kirafiki Toto vs Ndanda Fc waota mbawa

Mchezo wa kirafiki uliokuwa uchezwe leo kwenye dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza kati ya Toto Africans ya Mwanza na Ndanda Fc ya mkoani Mtwara hautachezwa kama ilivyokuwa imepangwa


Toto Africans ya mwanza
Wachezaji wa Toto Africans ya Mwanza

Taarifa za uhakika ambazo isaackwakuganda blog imezipata zinaeleza kuwa,Ndanda Fc ambayo inashiriki Ligi kuu soka Tanzania Bara imeitaarifu Toto Africans kuwa haitaweza kucheza mchezo huo kwasababu hawatakuwa na muda wa kutosha katika matayarisho yao ya mchezo ujao dhidi ya Mtibwa Sugar

Baada ya kupata ushindi kwenye mtanange wa juzi jumamosi-Septemba 20 kwa kuifunga Stand United ya Shinyanga kwa mabao 4-1 kwenye dimba la CCM Kambarage mkoani Shinyanga,jumamosi hii Septemba 28 itakuwa dimbani Manungu mkoani Morogoro kukipiga dhidi ya Mtibwa Sugar ambayo katika mchezo wake wa kwanza iliiduwaza Youngs Africans kwa mabao 2-0
Kwa upande wa Toto Africans  walitarajia kuutumia mtanange huo kama sehemu ya matayarisho kuelekea mashindano ya Ligi soka daraja la kwanza Tanzania Bara
[FDL[ambayo yataanza mapema mwezi ujao

Kwa sasa Wana-Kishamapanda hao wameweka kambi yao kwenye Chuo cha Ualimu Butimba jijini Mwanza
Kikosi cha timu ya Ndanda Fc ya mkoani Mtwara ambacho kinashiriki Ligi kuu soka Tanzania Bara


Share on Google Plus

About Unknown

"Is the CEO and Co-Founder of wakuganda in sports blog, dedicated to give you Sport roundups, updates, live scores and all sporting events,"
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment