Bayern Munich inasubiriwa na kikosi cha Hamburg SV kikiwa chini ya uongozi mpya leo jioni(20.09.2014)katika igi kuu ya Ujerumani Bundesliga.
Kocha wa Bayern Munich Pep Guardiola alibadilisha mtindo wake wa kucheza kwa mbinu ya mfumo wa 3-4-1-2 na kwenda katika mfumo wa 4-1-2-3 katikati ya mchezo ambao timu hiyo ilitoka na ushindi mwembamba nyumbani dhidi ya Manchester City , na mabadiliko hayo yalileta matunda , wakati Bayern ikicheza katika moja ya mchezo wake mgumu kabisa wa msimu huu, na kupata ushindi katika dakika ya 90 ambapo mlinzi Jerom Boateng alipachika bao la ushindi.
"Tulikuwa na matatizo kuudhibiti mpira , ndio sababu tulibadilisha kutoka ulinzi wa mabeki watatu na kuwatumia walinzi wanne," amesema Guardiola , ambaye hakutaka kusema atatumia mfumo gani dhidi ya Hamburg leo jioni(20.09.2014).
Hamburg ambayo iko mkiani mwa ligi ya Ujerumani Bundesliga ina matatizo yake binafsi, licha ya kuwa timu hiyo kutoka kaskazini mwa Ujerumani ina matumaini kwamba imetatua baadhi ya matatizo hayo kwa kumfuta kazi kocha Mirko Slomka baada ya kupata point moja tu na bila timu yake kufunga bao katika michezo mitatu ya ligi hiyo.
Kocha mpya ni kocha wa zamani wa kikosi cha vijana wa chini ya miaka 23 wa Hamburg Josef Zinnbauer.

0 comments:
Post a Comment