Olegunnar Solskjaer aachia ngazi Cardiff City


aliyekuwa Kocha Mkuu wa kikosi cha Cardiff City, Ole Gunnar Solskjaer ameachia ngazi.
Solskjaer, 41, ameachia ngazi baada ya kufanya mazungumzo na mwenyekiti wa klabu hiyo, Mehmet Dalman.

Cardiff hawakuwa na mwendo mzuri hata baada ya kuporomoka hadi daraja la kwanza.
Katika timu 20 wako katika nafasi ya 17 ikiwa ni baada ya kupoteza mechi sana mfululizo.
Mechi ya mwisho walifungwa juzi Jumanne, wakiwa nyumbani walilala kwa bao 1-0 dhidi ya Middlesbrough ikiwa ni siku chache baada ya kufungwa 4-2 dhidi ya Norwich.
Nafasi ya Ole sasa itashikiliwa na beki mkongwe Danny Gabbidon akisaidiana na Scott Young.
Ole, mshambuliaji nyota wa zamani wa Man United alichukuliwa ili kuisaidia klabu hiyo kuepuka kuteremka kutoka Ligi Kuu England, lakini ikashindikana.
Share on Google Plus

About Unknown

"Is the CEO and Co-Founder of wakuganda in sports blog, dedicated to give you Sport roundups, updates, live scores and all sporting events,"
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment