MCHEZO WA SIMBA NA YANGA KUSOGEZWA MBELE;WAMBURA ATAJA SABABU

Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, Boniface Wambura amewataka wapenda soka kuvuta subira hadi kesho ili kujua mechi ya watani iliyoondolewa Oktoba 12 itachezwa lini.

Boniface Wambura - Mkurugenzi wa mashindano TFF
Boniface Wambura - Mkurugenzi wa mashindano TFF

Lakini akasema hakuna chochote kilichosababisha zaidi ya uamuzi wa Benin kutaka kucheza Oktoba 12.
"Tulikuwa tunapambana kupata mechi, Benin waliona siku hiyo ndiyo wana nafasi.
"Ukizingatia imo ndani ya kalenda ya Fifa, sasa nafikiri hakuna kosa lolote," alisema Wambura.
"Watu wavute subira, tutawatangazia kesho lini mechi hiyo itachezwa. Usiku huu tunakwenda kukutana na bodi ya ligi kulijadili suala hilo."
Mashabiki wamekuwa wakilalamika kwamba kusogezwa kwa mechi hiyo kunaashiria kubebwa kwa Simba iliyokuwa ina wachezaji wengi majeruhi.
Share on Google Plus

About Unknown

"Is the CEO and Co-Founder of wakuganda in sports blog, dedicated to give you Sport roundups, updates, live scores and all sporting events,"
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment