Simba yajichimbia Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya ligi kuu bara

TIMU ya Simba inatarajiwa kuwasili Dar es Salaam Jumamosi hii kwa ajili ya mechiya Jumapili dhidi ya Coastal Union mchezo ambao utafanyika uwanja wa taifa Dar esSalaam.
Makamu wa rais wa Simba Geofrey Nyange Kaburu,ameviambia vyombo vya habari kuwa timu yao kwa sasa ipo Kambini Zanzibar ikiwa katika maandalizi ya mwisho kabla ya kuanza ligi hiyo Jumapili na wanamatumaini ya kutwaa ubingwa msimu huu kutokana na ubora wa kikosi walicho sajili.
“Tulipotoka Mtwara tulirudi Zanzibar kwa sababu tunaamini ndiyo sehemu ambayo inabahati kwetu hata 2010 tukiwa chini ya kocha Patrick Phiri,tuliweka kambi huku na tukawa mabingwa tena bila kufungwa,”anasema Kaburu.
Share on Google Plus

About Unknown

"Is the CEO and Co-Founder of wakuganda in sports blog, dedicated to give you Sport roundups, updates, live scores and all sporting events,"
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment