Msimu mpya 2014/2015 wa Ligi kuu soka ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), unatarajiwa kuanza kesho ambapo michezo sita itachezwa kwa timu 12 kushuka dimbani kuwania alama tatu muhimu.
Baada ya michezo 6 ya kesho, ligi hiyo itaendelea tena jumapili hii kwa mchezo mmoja kupigwa ili kuhitimisha raundi ya kwanza.
Ratiba na dondoo muhimu
| 1. AZAM FC | Vs | POLISI MOROGORO | AZAM COMPLEX | DAR ES SALAAM |
Mabingwa watetezi wa VPL Azam FC watafungua pazia dhidi ya timu iliyopanda daraja msimu huu ya Polisi Morogoro kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Azam Complex Dar - es - salaam.
Azam itaingia kwenye mchezo huo ikiwa na kumbukumbu ya kipigo cha mabao 3 - 0 toka kwa wana Jangwani kwenye mchezo wa ngao ya jamii uliochezwa jumapili iliyopita.
| 2. | MTIBWA SUGAR | Vs | YOUNG AFRICANS | JAMHURI | MOROGORO |
Mtanange wa pili utakua baina ya Mtibwa Sukari na makamu bingwa wa VPL msimu uliopita. Mtibwa ambao hawakufanya vizuri kwenye msimu uliopita wamejinasib kupitia kwa afisa habari wao Thobias Kifaru kwamba wako tayari kwa mchezo huo na wala hawaihofii Yanga.
Yanga kwa upande wao wataingia kwenye mchezo huo huku tayari wakiwa wameka kibindoni taji la ngao ya jamii baada ya kuigaragaza timu ya Azam FC mabao 3 - 0 juma lililopita.
Macho na masikio ya wanazi wa soka hapa nchini yataelekezwa kwa Mbrazil Jaja ambaye alifunga mabao 2 bora katika mchezo uliopita dhidi ya Azam FC kwenye ngao ya jamii.
| 3 | STAND UNITED | Vs | NDANDA FC | KAMBARAGE | SHINYANGA |
Timu zote mbili zinacheza kwa mara ya kwanza kwenye ligi kuu ya Tanzania Bara.
Stand United maarufu kwa jina la wanaamshaamsha, inatarajiwa kuendelea kuwa kivutio kikubwa kwa watu wa mkoa wa Shinyanga kutokana na kuwa timu ya wananchi. Timu hizo zote, tayari zimepata udhini wa kutosha mbali na udhamini wa Vodacom na Azam.
Mfano Stand United, inao udhamini wa mwaka mmoja na kampuni ya Binslum Tyres wenye thamani ya pesa ya kitanzania milioni 50 pamoja na udhmini wa Benki ya Exim.
| 4 | MGAMBO JKT | Vs | KAGERA SUGAR | MKWAKWANI | TANGA |
Mgambo JKT wataanzia nyumbai hapo kesho dhidi ya Wanasuper - nkurukumbi wa kagera huku ikikumbukwa vema jinsi ilivyoitibulia Yanga katika harakati za kuwania ubingwa msimu uliopita.
| 5 | RUVU SHOOTINGS | Vs | TANZANIA PRISONS | MABATINI | COAST REGION |
| 6 | MBEYA CITY | Vs | JKT RUVU | SOKOINE | MBEYA |
Mbeya City wanayo kazi ya ziada ya kuwadhihirishia Watanzania kwamba mafanikio waliyoyapata msimu uliopita haikuwa bahati bali uwezo wa timu.
Licha ya kuwa kikosi chao hakina mabadiriko makubwa, lakini kitendo cha hivi karibuni cha klabu hiyo kukubali kichapo cha mabao 4 - 1 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Vipers ya Uganda kimezua maswali mengi juu ya uwezo wa.
Kwa upnde wa JKT Ruvu chini ya kocha Fred Felix Kataraia Majeshi Minziro, inaonekana wazi wamejipanga ipasavyo kujiwinda na mchezo wa kesho na mingine itakayofuata.
| 7 | SIMBA SC | Vs | COASTAL UNION | NATIONAL STADIUM | DAR ES SALAAM |
Huu ni mchezo wa kuhitimisha raundi ya kwanza ya VPL ambao utachezwa jumapili hii ya septemba 21 kwenye uwanja wa Taifa Dar - es -salaam.

0 comments:
Post a Comment