Uongozi wa klabu ya Simba umesema sare ya mabao 2-2 dhidi ya Coastal Union, jana, haukuwa mzuri kwao lakini wameupokea kama changamoto.
![]() |
| Geofrey Nyange, Makamu Rais wa Simba |
“Hakuna aliyetarajia, inawezekana vijana wetu walijisahau baada ya kuongoza kwa mabao mawili wakaona tumeshinda.
“Kipindi cha pili Coastal Union wakajirekebisha na kucheza mchezo mzuri na kutupa wakati mgumu, mwisho wakasawazisha,” alisema Kaburu.
“Tayari tumeanza kambi Zanzibar na tutayatumia makosa ya mechi iliyopita kama sehemu kujiimarisha.”
Simba itacheza mechi ya pili dhidi ya Polisi Morogoro katika mechi itakayopigwa Jumamosi ijayo.

0 comments:
Post a Comment