Arsenal yang'ara ugenini, Ozil na Welbeck watakata

Arsenal yajitutumua ugeni kwa kuipiga Aston Villa 3 - 0. Matokeo hayo yamekuja baada ya kipigo cha 2 - 0 alichopokea kutoka kwa Dortmund katika ligi ya mabingwa Ulaya juma lililopita.


Danny Welbeck
Danny Welbeck akifunga bao dhidi ya Aston Villa


Arsenal ilionekana kuumudu mchezo vizuri baad ya Wenger kurudia mfumo wa  4-2-3-1. Walitawala sehemu ya kiungo iliyomilikiwa vyema na Arteta, Ramsey na Santiago Carzola.
Wachezaji wa Arsenal wakishangilia goli lililofungwa na Mesut Ozil dhidi ya Aston Villa


Bao la kwanza lilipachikwa na Mjerumani Mesut Ozili ambaye pia alimtengenezea  Danny Welbeck pasi nzuri aliyoisukumia kimiani bila hiyana.

Mchezaji wa Aston Villa Cissokho alijifunga baada ya kuunganisha krosi iliyomiminwa na Keran Gibbs na kuiandikia Arsenal bao la 3






Share on Google Plus

About Unknown

"Is the CEO and Co-Founder of wakuganda in sports blog, dedicated to give you Sport roundups, updates, live scores and all sporting events,"
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment