![]() |
| Stanslaus Mabula (wa pili kutoka kushoto) mstahiki Meya wa halmashali ya jiji la Mwanza akikabidhi vifaa kwa ajili ya pepsi - meya cup |
Mashindano
ya soka ya Pepsi kombe la Meya yatafikia tamati join ya leo kwa mtanange wa
fainali kupigwa kwenye dimba kongwe la Nyamagana jijini Mwanza kati ya timu ya
kata ya Mkolani na ile ya kata ya Mirongo.
Mchezo huo
wa fainali utatanguliwa na mchezo wa kutafuta nafasi ya tatu ambao
utazikutanisha timu za Mnadani na Sokoni.
Kwenye
fainali ya leo, Mkolani wanaonekana kupania zaidi kutwaa ubingwa wa mashindano
hayo kwani mwaka jana pia ambapo mashindano hayo yalianza, Mkolani ilitinga
fainali na kubamizwa na isamilo kwa mabao 2 – 1
Akizungumza na
isaackwakuganda.blogspot.com asubuhi ya leo, Mratibu wa mashindano hayo Mohammed
Bitegeko amesema kuwa , matayarisho yote kuelekea fainali ya leo yamekamilika
huku pia akisema kuwa mashindano ya mwaka huu yamekuwa bora zaidi ya yale ya
mwaka jana
“Kiukweli
mashindano yet yamekuwa mazuri sana, kwanza tuliongeza idadi ya viwanja vilivyotumika
ambapo tumetumia viwanja sita , tumetoa
vifaa vingi vya michezo kwa timu shiriki lakini kizuri zaidi tumetumia waamuzi Kutoka
kituo cha kukuza vipaji vya michezo cha Alliance jijini Mwanza” amesema
Bitegeko.
Zawadi za
washindi wa mashindano ya pepsi kombe la Meya kwa mwaka huu ni
Mshindi wa 01
- Bajaji ya kisasa ya mizigo thamani ml 4.5
- TSH. Ml 1.5
- Kombe
- Medali za dhahabu
Mshind wa 02
- TSH mil 3
- Medali za fedha
Mshindi wa 03
- TSH mil 2
- Medali za shaba
Timu yenye nidhamu
- Itaambulia THS 200,000/=
Mfungaji bora
- TSH 200,000/=
Mwalimu Bora
- TSH 200,000/=
Mashindano
hayo yamefanyika kwa mara ya pili mwaka huu yakishirikisha jumla ya timu 22
kutoka wilaya ya Nyamagana kutoka kata 12 za jimbo la Nyamagana na timu 10
kutoka katika makundi maalum
Mashindano
yalianza Agosti 02,2014 yakiwa chini ya udhamini wa kampuni ya SBC Tanzania
Limited kupitia kinywaji cha cha Pepsi, huku muasisi wa mashindano hayo akiwa
Mstahiki Meya wa Halmashauri ya jiji la Mwanza ambae pia ni diwani wa kata ya
Mkolani - Stanslaus Mabula

0 comments:
Post a Comment