Polisi nchini Uingereza wameanzisha uchunguzi kuhusu tukio ambalo mshambulizi wa Liverpool kutoka Italia Mario Balotelli alitukanwa kutokana na rangi ya ngozi yake kupitia kwa mtandao wa kijamii wa Twitter.
![]() |
| Mario Baloteli |
Polisi katika
mji wa Merseyside wameanzisha uchunguzi kufuatia matusi hayo yaliyotokea baada
ya mshambulizi huyo wa Liverpool kutuma ujumbe akiicheka Manchester United
kupokea kichapomikononi mwa timu ndogo ya Leicester siku ya jumapili.
Baloteli
aliandika ''Man Utd...LOL'' na ujumbe wake ukasambazwa zaidi ya mara 150,000 na
mashabiki wake.
Hata hivyo
miongoni mwa mwa wale waliouona ujumbe huo walimfokea kwa kuicheka United na
wakamtusi kwa misingi ya rangi yake.
Japo ni raiya
wa Italia Balotelli mwenye umri wa miaka 24 ana asili ya kiafrika.
Polisi tayari
wamefunga kurasa kadha zilizotuma jumbe hizo huku wakianza uchunguzi
waliozimiliki ni kina nani na wanaishi wapi iliwakamatwe na kujibu mashataka ya
ubaguzi wa rangi.
Kundi
linalopigania kumaliza ubaguzi wa rangi katika michezo Kick It Out lilisema
kuwa baada ya kuarifiwa kuwepo kwa matusi yenye kumdhalilisha Balotelli, kundi
hilo lilianzisha uchunguzi kwa ushirikiano na polisi wa mitandao ya kijamii.
Sio mara ya
kwanza kwa Mshambulizi huyo kudhulumiwa kwa misingi ya rangi yake .
Balotelli
ambaye alikuwa uwanjani Liverpool ilipolazwa 3-1 na West Ham jumamosi amewahi
kudhulumiwa kwa misingi ya rangi yake timu ya Italia ilipokuwa ikijifua kwa
kombe la dunia mwezi mei mwaka huu .
Awali pia
aliwahi kutukanwa akiwa Inter Milan na pia akihudumu AC milan.

0 comments:
Post a Comment