Ligi Kuu ya England inaendelea leo katika viwanja mbalimbali, huku kila timu ikisaka pointi tatu muhimu katika msimamo wa ligi hiyo.
![]() |
| mshambuliaji wa Liverpool "Super" Mario Baloteli |
Katika mchezo wa mapema Jumamosi,
Liverpool watakuwa wageni Newcastle katika mpambano huo. Katika rekodi
za nyuma Liverpool haijawahi kushindwa dhidi ya Newcastle katika mechi
nne walizokutana, Liverpool wakishinda mechi mbili na kutoka sare mechi
nyingine mbili. Hata hivyo hakujawahi kutokea sare ya bila kufungana
kati ya timu hizi katika mapambano 40 ya Premier League. Kwa mara ya
kwanza sare ya kutofungana kati ya Liverpool na New Castle ilikuwa mwezi
Februari 1974.
Timu ya Newcastle ilipoteza wachezaji watano kwa kupigwa kadi nyekundu katika michezo minne waliyokutana na Liverpool.
Katika
michezo tisa iliyochezwa na timu hizo katika ligi kuu ya England
inayoendelea, Liverpool inashika nafasi ya saba ikiwa na pointi 14, huku
Newcastle ikiwa katika katika nafasi ya 14 na pointi 10.
Michezo
mingine ya Jumamosi ni kati ya Arsenal na Burnley, Chelsea dhidi ya QPR,
Everton wakimenyana na Swansea, Hull wakipepetana na Southampton,
Leicester wakionyeshana kazi na West Brom, huku Stoke City wakinyukana
na West Ham.
Kati ya michezo itakayochezwa Jumapili, mechi
inayosubiriwa na mashabiki wengi duniani ni kati ya Manchester City
watakapovurugana na ndugu zao Manchester United. Manchester City
wanashikilia nafasi ya tatu wakiwa na pointi 17, huku Manchester United
wakiwa nafasi ya nane na pointi 13.
Mchezo mwingine ni kati ya Aston Villa na Tottenham.

0 comments:
Post a Comment