Uuzaji mchanganyiko wa
tiketi za elektroniki kwenye Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) utakoma baada ya mechi
mbili za wikiendi hii kati ya Yanga na Mgambo Shooting na Simba na Ruvu
Shooting zitakazochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Ligi itasimama kupisha
mechi ya Kalenda ya FIFA, mashindano ya Chalenji na dirisha dogo la usajili.
Baada ya hapo tiketi zote zitauzwa kwa njia ya mtandao, hivyo hakutakuwepo na
vibanda vya kuuza tiketi viwanjani.

0 comments:
Post a Comment