Klabu ya soka ya Toto Africans ya Mwanza ,imeendelea kujikita kileleni mwa msimamo wa Ligi soka daraja la kwanza[FDL]kwa upande wa kundi B baada ya hapo jana kutoka sare ya kufungana bao 1-1 na Polisi Mara kwenye dimba la Karume mjini Musoma mkoani Mara
| Nahodha wa Toto African (Kulia) akisalimiana na nahodha wa Polisi Mara Katika mchezo wao wa kwanza dimba la CCM Kirumba |
Kwa matokeo hayo,Wana- Kishamapanda
hao wamefikisha alama 16 hivyo kuendelea kubaki kileleni baada ya kucheza
michezo minane.Michezo mingine iliyochezwa hapo jana imeshuhudia sare kutawala
ambapo kwenye uwanja wa Ushirika mkoani Kilimanjaro,wenyeji Panone Fc
wametoka sare ya mabao 2-2 na JKT Oljoro huku Polisi Tabora ikitoka sare
ya 0-0 na Rhino Rangers kwenye dimba la Ali Hassan Mwinyi mkoani Tabora
Michezo mingine mitatu ya kundi B
itachezwa leo ambapo Geita Gold Sc itaikaribisha Green Warriors kwenye uwanja
wa Nyankumbu sekondari huku Mwadui Fc ikiikaribisha JKT Kanembwa kwenye
dimba la Mwadui mkoani Shinyanga.Wafunga buti wa Polisi Dodoma watakuwa
nyumbani Jamhuri mkoani Dodoma kucheza na Burkina Faso Fc ya mkoani Morogoro
Timu mbili zitakazoshika nafasi za
juu kwenye kundi B na mbili kutoka kundi A-zitafuzu kucheza Ligi kuu soka ya
Vodacom Tanzania Bara msimu wa mwaka 2014/2015
0 comments:
Post a Comment