TOTO AFRICANS YAZIDI KUJIKITA KILELENI

Samson Alfred ndiye aliyeleta raha jijini Mwanza kwa kupasia nyavu dakika ya 68 baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na mlinda mlango wa Panone Fc Benedict Haule kutokana na shuti kali lililomiminwa na Emmanuel Swita wa Toto Africa.

Baadhi ya wachezaji wa Toto Africans ya Jijini Mwanza
Mchezo ulikuwa wa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu.
Katika Dakika ya 41 Ayoub Reuben wa Panone Fc  alikosa bao la wazi baada ya shuti lake kuokolewa kwenye mstari wa gori na mrinda mlango wa Tot Africa.

Katika  Dakika ya 42 ya mchezo, Waziri Hamisi wa Toto Africa alikosa bao akiwa amebaki Yeye na mlinda mlango wa Panone Fc , Benedict Haule kwa shuti lake kupaa juu ya lango.
Timu zote ziliingia mapumziko zikiwa hazijatikisa nyavu kwenye lang la mwenzake

Vikosi vya timu hizo vilikuwa kama ifuatavyo

Kikosi cha Toto Africans:-
EricNgwengwe,BahatiMwanza,HamimAbdul,LadslausMbogo,Franck Kimath,Samson Alfred,Waziri Hamis,Mwita Kemoronge,William Joshua na Jafari  Mohamed. (Kocha mkuu - John Tegete)

Kikosi cha Panone Fc
BenedictHaule,OmaryMichael,LeonaldJacob,GodfreyMbunda,Godfrey Masubugu,Juma MgunyaRaymond Moye,Leonald Munyiga,Ayoub Reuben,Said Mohamed na Benson Milanzi.(Kocha Mkuu - Maka Mwalwisi)


Share on Google Plus

About Unknown

"Is the CEO and Co-Founder of wakuganda in sports blog, dedicated to give you Sport roundups, updates, live scores and all sporting events,"
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment